Akizungumza na paparazi wetu, Dude alisema amewahi
kubebeshwa unga na rafiki yake wa karibu ambaye hakumtaja jina na walikuwa
wakitokea Nairobi nchini Kenya kuja Tanzania.Alisema wakati wanaanza safari
alipewa koti la baridi na rafiki yake huyo, akalivaa kumbe ndani yake lilikuwa
limeshonewa pakti za unga.
Walisafiri kwa gari na kila walipokutana na polisi
wanaokagua hawakumkagua Dude kwani waliishia kupiga naye picha na kumsifia kwa
kazi yake mpaka alipofika jijini Dar es Salaam.
“Kila tulipokuwa tunakutana na polisi rafiki yangu
alikuwa akiwawahi na kuwaambia kwamba yupo na mimi ambapo walifurahia kuniona
na kupiga picha na mimi bila kunikagua chochote,” alisema Dude.
Baada ya kupita vizingiti vyote, waliingia jijini
Dar es Salaam maeneo ya Kinondoni Manyanya alipokuwa akiishi rafiki yake huyo
ambapo alimwambia avue koti, akaanza kufungua mzigo aliokuwa ameushonea kwa
ndani.
Dude alijikuta akishikwa na tumbo la kuhara kutokana
na mshtuko alioupata baada ya kuona rafiki yake huyo akitoa madawa ya kulevya.
“Jamaa alinipa shilingi elfu hamsini za Kenya na ni
baada ya kufika Dar ndipo niligundua kwamba nilikuwa nimebebeshwa unga lakini
yule jamaa alishakamatwa na anatumikia kifungo
nchini Pakistani,” alisema Dude.
Hata hivyo Dude aliwashauri mastaa wenzake
kuwa
makini na marafiki zao kwani siyo wote wanaokamatwa wamebeba unga kwa kujua bali wengine
wanabebeshwa tu bila kujua.
GPL

No comments:
Post a Comment