Mama yake na marehemu Hussein Mkieti aka ‘Sharo
Milionea’ .Makubwa! Mama mzazi wa aliyekuwa nyota wa filamu na muziki, marehemu
Hussein Mkieti ‘Sharo Milionea’ amemtuhumu msanii wa vichekesho ambaye alikuwa
rafiki wa mwanaye, Musa Kitale kuwa alikula michango ya kumbukumbu ya kifo cha
mwanaye, mwaka jana.
Kwa mujibu wa chanzo makini, Mama Sharo amekuwa
akimlalamikia Kitale kwa watu kwamba alikula fedha za mchango wa mwanaye hivyo
kupigwa marufuku kwamba kitu chochote kinachomhusu Sharo asipewe.
Ilidaiwa kwamba, chanzo cha mama Sharo kutaka Kitale
asipewe kitu chochote kinachomhusu marehemu ni baada ya hivi karibuni Klabu ya
Bongo Movie Unity kutangaza kuwa litatoa Tuzo kwa Sharo Milionea kama
kumbukumbu kwani alikuwa ni mwenzao katika tasnia ya filamu.
Ilisemekana kuwa mama huyo alielezwa kwamba tuzo
hiyo itapokelewa na Kitale ndipo alipokataa na kusema hataki kabisa kitu
chochote kipitie kwa msanii huyo kwa sababu huwa hamfikishii.
Msanii wa vichekesho Musa Kitale.“Mama Sharo amekuwa
akilalamika kwa muda mrefu sana kwamba Kitale anatumia vitu vya mwanaye, eti
alichangisha michango ya kumbukumbu hakumfikishia hivyo kwa sasa ameamua kupiga
marufuku asikabidhiwe kitu chochote,” kilisema chanzo hicho.
Baada ya kupata habari hizo, wanahabari wetu
walimtafuta Kitale ambapo kabla hata ya kujibu tuhuma hizo, alinyanyua simu na
kumpigia mama Sharo kumuuliza kama kweli amezungumza madai hayo.
Mama Sharo alikiri kuwa ni kweli alizungumza akidai
alifikia uamuzi huo baada ya kutonywa na watu kuwa Kitale amekuwa
‘akichikichia’ fedha za marehemu mwanaye.
Kitale, baada ya kujiridhisha, alitoa ufafanuzi kuwa
madai hayo hayana ukweli na kudadavua kwamba wakati wa kumbukumbu ya Sharo
mwaka mmoja (Novemba) tangu alipofariki dunia, hakuna michango yoyote
iliyotolewa.
“Inaniuma sana kwa sababu enzi za uhai wa Sharo
hatukuwahi kugombana hata siku moja na mama Sharo alikuwa analitambua hilo,
tuliishi kama ndugu na mimi ndiye niliyemsaidia mpaka akapata umaarufu lakini
sasa namshangaa huyu mama kunishutumu vitu vya uongo,” alisema Kitale kwa
huzuni huku jasho likimtiririka.
No comments:
Post a Comment