Huwezi amini pamoja na utajiri alionao, Jose Chameleone amenyang’anywa gari yake aina ya Escalade na
maofisa wa URA baada ya mamlaka hiyo kudai kwamba msanii huyo ameshindwa kulipa
kodi yenye thamani ya shilingi milioni saba ya Uganda.
Muda mchache kabla ya kuanza kwa onyesho kubwa la Tubonge la
msanii huyo, maofisa wa URA waliikamata gari yake hiyo ya kifahari.
Kwa mujibu wa mtandao wa Redpapper wa nchini Uganda,msanii
huyo alijaribu kuwakatalia wasikuchukue gari lake akidai atakufa na mtu
atakayeichukua lakini kauli hiyo haikufua dafu kwa mamlaka hiyo. “Hii ni gari
yangu binafsi na nina haki yake, mtu yeyote akigusa Escalade yangu, nami tufe
pamoja naye,” alidai Chameleone.
Hata hivyo Chameleone alidai kuwa hana tatizo lolote kulipa
kodi lakini mamlaka hiyo haikutolea vigezo walivyotumia kupata jumla ya
shilingi milioni 7 za Uganda ambazo ndizo pesa wanazomdai.
No comments:
Post a Comment