Kwa mujibu wa chanzo chetu, Rose alidakwa jijini Dar es
Salaam saa sita mchana huku mlalamikaji wake akiwa ni mtu aliyejulikana kwa
jina la Nathan Wami.
Nathan amewahi kuwa meneja wa kazi za Rose Muhando. Kwa sasa
Rose anaratibiwa na Kampuni ya Sony.
MADAI YA JALADA LA KESI
Kwa mujibu wa chanzo, jalada la kesi hiyo lilifunguliwa
Dodoma likisomeka; DOM/RB/1129/2014 KUJIPATIA MALI KWA NJIA YA UDANGANYIFU.
Hata hivyo, ilidaiwa kuwa Rose aliachiwa kwa dhamana
akitakiwa kurudi kituoni hapo Februari 8, 2014 huku mkononi akiwa ameshika
kiasi hicho cha fedha kwa ajili ya kumlipa mlalamikaji huyo.
WIKIENDA LATINGA POLISI MSIMBAZI
Baada ya kuinyaka nyeti hiyo, Ijumaa Wikienda lilipiga hodi
kituoni hapo na kuulizia kama ni kweli nyota huyo wa wimbo wa Utamu wa Yesu
alishikiliwa.
“Sisi si wasemaji wakuu wa polisi, hatuna mamlaka hayo.
Hatuwezi kusema ni kweli au si kweli,” afande mmoja alilijibu gazeti hili.
MADAI NYUMA YA PAZIA
Wakati madai ya Rose yakiwa hayo, nyuma ya pazia kuna
mlolongo wa matukio ya kushangaza kati ya mwimbaji huyo na Nathan.
Kwa mujibu wa chanzo kimoja, Rose amekuwa akiingia kwenye
madai ya kupokea fedha za shoo na kutokwenda lakini Nathan akielekezewa lawama
zote.
PESA APOKEE MENEJA, LAWAMA ABEBESHWE ROSE
“Jamani mimi nataka kuwaambia ukweli, Rose hahusiki na hiyo
tabia. Wengi wanasema ana mchezo wa kuchukua fedha za watu halafu haendi kwenye
tukio lakini ukweli si huo,” kilisema chanzo hicho.
Wikienda: “Ukweli ni upi? Funguka basi.”
Chanzo: “Ukweli ni kwamba, Nathan amekuwa akimnyanyasa sana
Rose kwa muda wote aliokuwa meneja wake.
“Ilifika mahali,
Nathan ndiye alikuwa akipokea pesa kutoka kwa watu wanaomhitaji Rose bila
kuwasiliana na mwenyewe. Wakati mwingine Rose hajulishwi mapema.
“Siku akiambiwa, pengine anaumwa au yupo mbali na eneo la
tukio, sasa hapo waandaaji wanamsema Rose kwamba amechukua fedha na kuingia
mitini,” chanzo kilizidi kuweka wazi.
ROSE HANA CHA KUFANYA
Kwa mujibu wa chanzo, hali hiyo imekuwa ikimsumbua sana Rose
kwani ni kweli wengi wanaamini hivyo lakini ukweli ni kwamba anasingiziwa tu,
Rose hawezi kupokea fedha halafu asiende kuimba ila kwa sababu Nathan ni meneja
wake aliyemtoa kisanii anajikuta hana la kufanya.
“Mbona kwenye
matamasha ya Pasaka na Krismasi yanayoandaliwa na Msama Promotion hatujawahi
kusikia Rose kaingia mitini? Ni kwa sababu Msama mwenyewe anawasiliana naye
moja kwa moja,” kiliendelea chanzo.
NATHAN ALIISHI NA ROSE KWA UBABE
Ikazidi kudaiwa na chanzo chetu kwamba katika kipindi chote,
Nathan amekuwa akiishi na Rose kwa ubabe wa hali ya juu, jambo ambalo
lilimuathiri Rose kisaikolojia bila kujijua.
“Kuna mengi sana, tena yale ya ndani zaidi, sipendi kuyasema
lakini Nathan mwenyewe anayajua, siku ikifika nitayalipua kama atapinga,”
kilisema chanzo.
ROSE MUHANDO HUYU HAPA
Ijumaa Wikienda lilimtafuta Rose kwa lengo la kutaka
kumsikia atakachokisema juu ya madai yote hayo kuhusu yeye na Nathan, lakini
zaidi ya yote tukio la kuwekwa mahabusu ya Msimbazi Polisi, msikie:
“Kusema ule ukweli mimi namwachia Mungu, yeye anajua ukweli
uko wapi na uongo uko wapi!”
NATHAN SASA
Baada ya hapo, gazeti hili lilimtafuta Nathan Wami na
kumsomea mashitaka yote.
Nathan: “Hayo madai si ya kweli. Kama kasema yeye siyo
kweli. Nimeishi na Rose karibu miaka kumi na mbili, nilikuwa namchukulia kama mtoto
wangu.
“Nimekuwa nikiona kwenye magazeti kwamba eti alisaidiwa na
mfuko wa kanisa wakati mimi ndiye niliyemtoa.”
Wikienda: “Kwa hiyo
madai kwamba umekuwa ukiishi naye kibabe, hukuwa unamtendea haki si ya kweli?”
Nathan: “Si ya kweli hata kidogo.”
MSAMA ANAMLIPA NANI?
Gazeti hili liliwasiliana na muandaaji wa matamasha ya
Pasaka na Krismasi, Alex Msama kuhusu malipo ya Rose Muhando.
Msama: “Mimi huwa namalizana na Rose.”
Wikienda: “Kuna mwaka umewahi kumlipa pesa halafu hakutokea
kwenye tamasha lako?”
Msama: “Hapana, hata Tamasha la Pasaka mwaka huu atakuwepo
panapo uzima maana tumeshamalizana.”
KUTOKA KAMPUNI YA SONY
Habari zilizopatikana kutoka Kampuni ya Sony ambayo
inamratibu Rose kwa sasa, zinasema kuwa wakati wa kuingia makubaliano na nyota
huyo walikutana na masuala hayo ya madeni lakini walipofanya uchunguzi
wakagundua mambo ambayo hawakutaka kuyaweka wazi lakini kimsingi walimhurumia
Rose.
“Ila mabosi wa Sony
waliamua kuwa yale madeni yaliyopita watayalipa wao, yale ambayo tarehe za Rose
kuimba bado, wamemwambia akaimbe ili kumalizana na wahusika,” kilisema chanzo
hicho na kuomba kutotajwa jina
No comments:
Post a Comment