VITU VYA AJABU NDANI YA KONTENA |
Wamiliki wa supermarket ya Village Market ya nchini Kenya wamejitokeza
na kudai kuwa vitu vilivyokuwa kwenye kontena lilikamatwa Mombasa ni vya kwao.
Wamesema waliagiza vitu hivyo kutoka China kwaajili ya
sikukuu ya Kimarekani ya Halloween baadaye mwezi huu.
Katika maelezo yake, wameandika:
Market Masters LTD, hereby confirms that indeed we have
ordered for the Halloween decorative items imported from China in container
number PCIU 8125750, and are not restricted items.
Just like during Easter Holiday or Christmas season, the
items in question are solely used for decorating the entire shopping centre for
our annual Halloween parties held within village market every last Saturday in
October, for the past 17 years.
We needed to replace the old worn out ones with us, in
readiness for our upcoming Haloween party slated for 26th October 2013.”
Kontena hilo lilikuwa na wanasesele wa kutisha, wanaonekana
wakiwa na maumivu makali, mikono na miguu iliyokatwa, maiti na vitu vingine
vilivyodaiwa kuwa vya kishetani.
Awali, vitu hivyo vilidaiwa kuwa vya mwanasiasa maarufu wa
Kenya, aliyewahi kuwa naibu waziri wa zamani, Omingo Magara ambaye alilazimika
kujitokeza na kukanusha japo alikiri kuwa baadhi ya vitu vyake (tofauti kabisa
na vitu hivyo vya ajabu) vilikuwemo ndani ya kontena hilo.
Na sasa ameitaka mamlaka ya mapato nchini humo, KRA kumwomba
radhi na kama ikishindwa ndani ya siku 7 ataipeleka mahakamani.
No comments:
Post a Comment