MSHAMBULIAJI Mrisho Ngassa wa Yanga, ameuambia uongozi wake
yupo tayari ulilipe Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kitita cha Sh milioni 45
kutoka kwenye mshahara wake.
Ngassa amekubali kitita hicho cha fedha kitolewe kwa kuwa
ana hamu ya kuanza kuitumikia Yanga baada ya kumaliza adhabu ya kutocheza mechi
sita aliyopewa na TFF.
Imeelezwa Ngassa yupo tayari kukatwa katika mshahara wake na
kuna taarifa katika Sh milioni 2 kila mwezi, atakatwa Sh 500,000.
Mshambuliaji huyo alisimamishwa mechi sita pamoja na kutakiwa
kurudisha Sh milioni 30 alizolipwa na Simba pamoja na faini ya Sh milioni 15.
TFF ilishikilia msimamo wake kwamba Ngassa hatacheza hadi atakapolipa fedha
hizo za Simba.
Habari za uhakika kutoka ndani ya Yanga zimeeleza kuwa,
Ngassa amekubali kuhusiana na hilo na alifikia makubaliano hayo na mwenyekiti,
Yusuf Manji walipofanya kikao walipokutana jijini Mbeya, hivi karibuni.
Alipoulizwa kuhusiana na hilo jana, Ngassa alisema: “Sawa, adhabu yangu ya kutocheza mechi sita
za mashindano imemalizika, lakini siwezi kuongelea lolote, mimi ni mchezaji tu,
kazi yangu ni ndani ya uwanja, hayo mengine ya kiutawala ni vyema yakatolewa ufafanuzi
na viongozi,” alisema Ngassa.
Championi Jumatano lilimtafuta Manji ambaye alikiri
kuzungumza na Ngassa kuhusiana na masuala kadhaa ya klabu yao likiwemo hilo.
“Mimi ni mwenyekiti, hakuna ubaya kuzungumza na Ngassa.
Tunazungumza kwa ajili ya klabu yetu, hivyo msubiri akicheza
mtamuona,” alisema Manji.
Taarifa nyingine zilieleza kuwa, Yanga ilikuwa tayari
kupeleka fedha hizo leo, lakini ilitaka TFF wakate Sh milioni 45 katika Sh
milioni 70 inazowadai na walikuwa katika mazungumzo katika hilo.
Kwa upande mwingine, Kocha Mkuu, Ernie Brandts, alisisitiza
kwamba ana kila sababu ya kumpanga Ngassa kama atakuwa amerejea katika kikosi
watakapoivaa Ruvu Shooting Jumamosi.
“Tuko naye kikosini kila siku, tunafanya naye mazoezi na
tunashirikiana. Kama amerejea na yuko katika afya nzuri, nitampanga maana
ninamhitaji,” alisema Brandts.
Wakati hilo la Ngassa linamalizika, taarifa nyingine za
uhakika zimeeleza Manji alitarajia kukutana na kikosi kizima cha Yanga, jana
usiku.
Mwenyekiti huyo alipanga kukutana na wachezaji na benchi la
ufundi katika hoteli ya Serena jijini Dar ili kula chakula cha usiku na baadaye
kujadili masuala kadhaa kikiwemo kipigo cha Azam FC na nini cha kufanya baada
ya hapo ili kusonga mbele na ikiwezekana kutetea
No comments:
Post a Comment