KWA NINI WASANII WANAOPOTEZA DIRA NA KUANGUKIA MAISHA MAGUMU
WANAONGEZEKA?
HALI HALISI YA WASANII
Kutokana na matukio kadhaa yanayowapata wasanii wa mziki wa
kizazi kipya, imenilazimu kufuatilia kwa makini maisha na mwenendo mzima wa
wasanii. Lengo langu lilikuwa ni kutaka kujua sababu zinazowafanya wasanii
kupoteza dira na kuangukia maisha magumu. Kwa haraka unaweza kujua kwamba hali
hii hutokea pale wasanii hao
wanapoanguka kisanaa na kujikuta kukosa kipato kikubwa amabcho walikuwa
wanakipata katika sanaa kipindi cha nyuma.
Mpaka sasa kuna wasanii kadhaa ambapo wengine wametangulia
katika haki na wengine wapo katka maisha magumu yenye muambatano na mambo
lukuki kama vile kujingiza katika matumizi ya madawa ya kulevya, kutumia
pombe/sigara kupita kiasi na hata kujihusisha na biashara haramu. Wasanai hao
wanajikuta wanaopoteza dira na kufa au kusubiri kufa huku vifo vyao
vikihusishwa na mambo hayo niliyoyataja(madawa ya kulevya n.k).
SABABU ZA WASANII KUANGUKA NA KUPOTEZA DIRA
Yawezekana zikawa sababu nyingi sana za wasanii kupotea na
kuanguka vibaya katika mziki lakini zifuatazo zaweza kuwa ni moja ya sababu za
msingi.
1. Kuwa na uwezo mdogo wa kufikiri au kukosa elimu ya
kawaida ya kuendesha maisha yao.
Wasanii wengi wanaingia katika mziki kwa kuwa wamejaliwa
kipaji cha kuimba ila wengi wao hawana aidha uwezo madhubuti au elimu ya kuweza
kufikiria wanafanya nini, wafanyeje, wanafanya kwa ajili gani, wanategemea
nini, na wanachokifanya kinafanyweje? Hali hii hupelekea wasanii hao kufanya
sanaa kwa kubahatisha na kubabaisha. Kwa hiyo mpaka mwisho wa siku anaposhuka
au kuanguka kisanaa mwenyewe anashindwa kujua ni kitu kipi kimemfanya aporomoke
na kitu gani afanye ili aweze kurudi kisanaa. Hali hii pia inapelekea wasanii
kutosimama kidete kudai haki zao pale zinapopokonywa, kutoshirikiana na kuunda
hata chama chao kitakachosimamia maslai yao kisheria. Mfano, utakuta tamasa
moja, wasanii wawili wenye uwezo sawa wanalipwa kiasi tofauti. Huku ni kukosa
ushirikiano na formality katika kazi yao.
2. Kuendekeza mitazamo isiyo na maana wanayoikuta katika
ulimwengu wa sanaa kutoka kwa wasanii
waliotoka kabla yao.
Kuna mambo mengi ambayo sio ya msingi yanayofanywa na
wasanii wengi na kuyafanya mambo hayo kama sehemu ya utamaduni wa wasanii
mfano; kabla ya kupanda stejini lazima uvute bangi, msanii lazima awe na
wasichana wengi, msanii kutotumia public services kama vile kupanda daladala
nk., msanii kufanya shopping au kula sehemu za matawi ya juu, msanii kuvaa kwa
jinsi fulani kama vile mlege(kwa wavulana) na nusu uchi (kwa wasichan). Mambo
hayo yote yanapelekea wasanii wengi wanaoingia katika game kuiga pasipo kuangalia
uwezo wao na madhara ya kufanya mambo hayo. Mwisho wa siku akiyumba kidogo tu
katika sanaa anapata pigo moja kubwa sana kwa kuwa anakuwa hana uwezo wa kuishi
kama alivyozoea. Hatimaye msanii huyo hupatwa na msongo wa mawazo na kuamua
kujiingiza katika madawa ya kulevya/pombe za kupindukia eti ili kuondoa STRESS.
3.Kutowekeza katika miradi mingine yoyote
Hili ni kosa lingine kubwa linalofanywa na wasanii wengi.
Mara wanapokuwa kileleni wanajisahau kwamba kuna wengine wanatamani kuwa katika
killele hicho, hivyo wanajitahidi kwa hali na mali kufikia hapo walipo. Tena
jitihada zinazofanywa na hao ni kubwa mno, na siku wakija kufika katika kilele
hicho, wanakuwa na hasira sana kiasi kinachopelekea spidi yao kuwa kubwa sana
na kumfanya yule aliye kileleni mara ya kwanza kushuka kwa spidi. Wasanii
hudhani kwamba wanapokuwa juu kisanii basi wataendelea kuwa hivyo milele yote,
kitu amabacho sio cha kweli. Wangekumbuka kubuni na kuwekeza katika miradi
mingine ili wanaposhuka katika game wasihangaika kimaisha kwa kuwa wangepata
kipato kinginge kupitia miradi yao.
Imeandikwa na:
Issaya Lupogo
Contact/Email: lupogoissaya@gmail.com

No comments:
Post a Comment